Wa Moyoni Wengi Wapo Kwa Wasio wa Moyoni
MPENZI msomaji nakukaribisha katika siku nyingine mwanana ya Jumanne ambayo tumeifikia kwa kudura za Mwenyezi Mungu. Tunakutana tena katika kujadili namna maisha ya kawaida na mapenzi yanavyoenda. Mada yangu ya leo itazungumzia namna ambavyo mtu anakuwa amemuweka mpenzi wake moyoni kwa kumjali, kumthamini, kumpenda, kumnyenyekea na namna yoyote ile ilimradi tu ni yenye kuonesha kuwa kweli ana upendo wa dhati kwa mpenzi wake huyo. Lakini cha ajabu, bila kujua kuwa anayempenda na kumthamini wala hajamuweka kabisa moyoni mwake bali na yeye amemuweka moyoni mtu mwingine kabisaaa! Mapenzi ya ajabu Ama kweli mapenzi ni kitu cha ajabu sana, nilichokibaini katika uchunguzi mfupi nilioufanya nimebaini kuwa wapenzi walio na mapenzi ya dhati kwa wapenzi wao, kiukweli wapenzi wao wengi huwa hawana mapenzi ya dhati kwao kama wanavyodhani bali wanaowapenda wanamapenzi na watu wengine. Ushahidi Ninaamini ulishawahi kukutana na kisanga cha jamaa au mdada kumlilia na kumbembeleza mpenzi wake ten...