Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Makontena 115 Ya Sukari Yanaswa Jijini Dar es Salaam....RC Makonda Aviagiza Vyombo vya Dola Vifanye Uchunguzi wa Kina

Makontena 115 Ya Sukari Yanaswa Jijini Dar es Salaam....RC Makonda Aviagiza Vyombo vya Dola Vifanye Uchunguzi wa Kina

Picha
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameagiza kuchunguzwa kwa sukari kontena 115 ambayo ni zaidi ya tani 3,000 iliyokutwa katika bandari kavu ya PMM iliyopo eneo la Vingunguti.  Makonda alitoa agizo hilo jana wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika bandari hiyo na kubaini uwepo wa sukari hiyo ambayo ni mali ya Mohamed Enterprises, ambayo kwa taarifa zake aliambiwa zilikuwa kontena 165.  Alisema anazitaka mamlaka zinazohusika kama Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), pamoja na Shirika la Viwango (TBS) kuichunguza sukari hiyo kutokana na sababu mbalimbali zilizojitokeza katika uwepo wa sukari hiyo kama sukari kuagizwa kutoka Dubai lakini imetoka Brazil na imepakiwa Dubai, na upangwaji wa kontena hizo katika bandari hiyo.  “Nashindwa kuelewa kwa nini sukari iagizwe kutoka Dubai lakini itoke Brazil na kufungashwa Dubai inaonesha inaweza kuwa imeshawahi kuisha muda wake hivyo nataka ichunguzwe na tunatak...