HASSAN RAMADHANI KESSY APEWA RUKSA KUONDOKA SIMBA
Na Moshi Shaban Baada ya tukio lililotokea kwenye mchezo wa Simba na Toto African la golikipa wa Simba Vicent Agban kumpiga beki wa kulia wa timu hiyo Hassan Ramadhani Kessy mambo yamebadilika kwenye timu hiyo na huenda yakawa makubwa zaidi kutokana na hali ilivyosasa. Uongozi wa klabu ya Simba umemwambia beki wake wa kulia Hassan Ramadhani ‘Kessy’ anaweza kuondoka kwenye timu yao baada ya mchezaji huyo kusema hatoendelea kuichezea timu hiyo tena kufuatia kupigwa na kipa Mu-Ivory Coast Vicent Agban baada ya mchezaji huyo kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika mchezo wa Ligi ya Vodacom dhidi ya Toto Africans. Mkataba wa beki huyo kuihudumia Simba umebakiza mwezi mmoja na kwa hali ilivyo kunauwezekano mkubwa ataondoka kutafuta timu nyingine ya kucheza zikiwemo Yanga au Azam. Msemaji wa Simba Hajji Manara, amesema mchezaji huyo anaweza kwenda kwasababu wamechoshwa na mambo yake na Simba haimtegemei yeye hivyo anaweza kuondoka na timu yao bado ikafanya vizuri kwenye mechi z...