Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya dalili na matibabu yake.

Maana ya Mafua, chanzo, dalili na matibabu yake.

Picha
Ugonjwa wa mafua unaweza kusababisha hali ya kupiga chafya mara kwa mara, kutokwa na makamasi mepesi au mazito puani, kikohozi, homa kali, na kuziba kwa pua. Mafua yanaweza kuwa moja ya sababu kubwa inayofanya watu wengi kushindwa kwenda kazini, katika shughuli mbalimbali za uzalishaji au kuhudhuria shuleni na kwenda kutafuta msaada wa kitabibu hospitalini.  Ingawa dalili za mafua siyo kali sana na hazidumu kwa zaidi ya majuma matatu, Shirika la Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa la Marekani (CDC) linasema kuwa, kila mwaka mafua husababisha kupotea kwa siku milioni 22 za mahudhurio shuleni nchini Marekani. Katika utafiti wao Fendrick AM, Monto AS, Nightengale B na Sarnes M uliochapishwa katika jarida la kitabibu la Archival of Internal Medicine toleo la 163 mwaka 2003, walibaini kuwa mafua yanaweza kusababisha mzigo mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi. Utafiti huo uliohusisha kaya 4,051 huko Marekani, ulionyesha kuwa takribani dola bilioni 40 za Marekani hupotea kila mwaka kutokana...