Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kutumia Bajaji na Bodaboda

Ofisi ya Waziri Mkuu Kutumia Bajaji na Bodaboda

Picha
Ofisi ya Waziri Mkuu itatumia usafiri wa bajaji na bodaboda kuendesha shughuli zake kuanzia mwaka ujao wa fedha wa 2016/2017 ikiwa ni mkakati wa kubana matumizi wa Serikali ya Awamu ya Tano. Mpango huo umo kwenye hotuba ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu iliyosomwa jana bungeni na Kassim Majaliwa, na baadaye kusifiwa na mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria ya Bunge, Mohamed Mchengerwa wakati akisoma maoni ya kamati kuhusu bajeti hiyo. Wizara iliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ni ya Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Walemavu. Akiwasilisha maoni ya kamati hiyo, Mchengerwa alisema uamuzi wa aina hiyo unaendana na dhana ya kubana matumizi ya fedha wa Serikali ya Awamu ya Tano. Hata hivyo, hotuba iliyosomwa na Waziri Majaliwa haijaeleza pikipiki hizo za magurumu mawili na matatu zitatumiwa na watumishi wa kada gani. Serikali ya Awamu ya Tano imekuwa kwenye mkakati mkali wa kubana matumizi yasiyo ya lazima na tayari Rais John Magufuli ametangaza kuwa kuanzia mwaka mp...