Rais Magufuli Asamehe Wafungwa 3,551
Rais John Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa 3,551, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya Muungano wa Tanzania. Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Meja Jenerali Projest Rwegasira ilisema wafungwa 580 wataachiwa huru, huku wengine 2,971 watapunguziwa moja ya sita ya vifungo vyao. Alisema rais ametoa msamaha huo kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya ibara ya 45(1)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aliwataja watakaonufaika na msamaha huo kuwa ni wafungwa wenye ugonjwa wa ukimwi, kifua kikuu na saratani ambao wapo kwenye hatua za mwisho. Wengine ni wazee wenye umri wa miaka 70 na kuendelea, wajawazito na wale waliongia na watoto gerezani. Wafungwa wengine watakaonufaika na msamaha huo ni wenye ulemavu wa akili ambao wamethibishwa na jopo la waganga kuwa wana tatizo hilo. Katibu mkuu wa wizara hiyo alisema msamaha huo hautawagusa wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa au kifungo cha maisha jela. Pia, wafungwa wanaotumi...