HOMA YA TUMBO (TYPHOID FEVER)
HOMA YA TUMBO (TYPHOID FEVER) Homa ya tumbo ikijulikana kama Typhoid fever kwa kiingereza ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria aina ya Salmoneilla typhi. Hii ni homa hatari inayoweza kuathiri ogani nyingi mwilini, na huambukizwa hasa kwa njia ya chakula. Jinsi Ugonjwa Unavyotokea Ugonjwa wa homa ya tumbo husababishwa na bakteria aina ya Salmoneilla typhi na Salmoneilla paratyphi . Ugonjwa huu huambukizwa kwa njia ya kula chakula au maji yenye vijududu hivi. Baada ya bakteria kuingia kwenye mwili kupitia maji au chakula, huvamia utumbo mdogo na kuingia kwenye mishipa ya damu. Huingia kwenye bandama, ini na ute wa damu na kuzaliana na baadae kuingia kwenye mishipa ya damu tena. Hapa ndipo homa na dalili nyingine huanza. Huendelea kusambaa kwenye utumbo, kongosho na mishipa ya limfu. Dalili Dalili za homa ya tumbo huanza kujionesha siku 7 – 14 baada ya vijidudu kuingia mwilini na ugonjwa kudumu kwa wiki 2 mpaka 4.. Dalili za homa ya tumbo hujumuisha HomaKukosa ha...