Lulu Afunguka, Mama Kanumba Ajibu
STAA wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ anadaiwa kulinogesha bifu lake na mama wa aliyekuwa nguli wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegeo kufuatia posti yake ya hivi karibuni akiashiria kumtisha mama huyo. Lulu juzikati alitupia ujumbe mtandaoni akimjibu mmoja wa mashabiki wake aliyeuliza sababu ya yeye na mama Kanumba kutoiva ambapo aliandika: “…ni hivi mimi siyo chizi jamani kila ninachokifanya nakijua vizuri tu, mimi ndo’ najua ‘what’s going inside’ (nini kinachoendelea) nyinyi wa nje yasikieni hivyohivyo, sitajibu watu wala mhusika mwenyewe ila siku ikifika nitaongea.” Baada ya kupostiwa kwa ujumbe huo, mashabiki walimjia juu Lulu wakieleza kuwa, hana sababu ya kumtisha mama Kanumba badala yake kama kuna lililo moyoni mwake aliseme kuliko kukaa kimya. “Huku sasa ni kumtisha mama wa watu, kama analo jambo aliseme watu wajue sababu ya bifu lao,” alisema mmoja wa mashab...