Upinzani dhidi ya uingiliaji wa kijeshi wa Magharibi nchini Libya
Sanjari na upinzani wa baadhi ya nchi za Kiarabu dhidi ya uingiliaji wa kijeshi wa Magharibi katika mgogoro wa Libya, Waziri wa Afya wa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika ametoa indhari kuhusiana na kutokea maafa ya kibinadamu katika nchi hiyo.Katika hali ambayo baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti kuhusiana na uwepo wa vikosi vya Ufaransa, Marekani, Uingereza na Italia katika ardhi ya Libya, Kanali ya Televisheni ya al-Jazeera ya Qatar imetangaza baada ya kufanya uchunguzi wa maoni kwa watazamaji wake kwamba, asilimia 90 ya watazamaji hao wanapinga nchi za Magharibi kuishambulia kijeshi Libya. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, baada ya Marekani kuishambulia kijeshi Afghanistan na Iraq na kuibuka makundi ya kigaidi na kitakfiri katika nchi za Afghanistan, Syria na Iraq wananchi wa nchi za Kiislamu hawana mtazamo mzuri kuhusiana na uingiliaji wa kijeshi wa madola ya Magharibi katika nchi za Mashariki ya Kati.Ramtane Lamamra, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Algeria kwa mara nyingine tena amet...