Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Mbunge Apewa Siku 3 Atoe Ushahidi wa Magari 777 ya Washawasha

Mbunge Apewa Siku 3 Atoe Ushahidi wa Magari 777 ya Washawasha

Picha
SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amempa siku tatu Mbunge wa Viti Maalumu, Susan Lyimo (Chadema) awasilishe mbele ya Kamati ya Maadili ya Bunge, maelezo ya utetezi dhidi ya madai aliyotoa bungeni kuhusu Serikali kununua magari ya washawasha 777.  Ndugai alitoa amri hiyo kutokana na mwongozo ulioombwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yussuf Masauni juzi akitaka Lyimo athibitishe au afute kauli yake juu ya madai hayo wakati serikali imenunua magari 32.  “Hata kwa akili ya kawaida haiwezekani Serikali ikaagiza magari yote hayo 777 ya washawasha. Ninachokumbuka mimi Waziri huyu aliwahi kusema hapa bungeni kuwa magari hayo 777 ni idadi ya magari yote ya aina mbalimbali yaliyonunuliwa kwa ajili ya matumizi ya polisi,” alisisitiza Ndugai.  “Sasa nakutaka uniandikie rasmi majibu vizuri kuhusu kauli yako hii, nakupa siku tatu uwe umeniletea na baadaye nitaipeleka taarifa yako kwa Kamati ya Maadili ya Bunge, ili kujadili suala hili kwa mapana,”...