Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya MATCH PREVIEW: NI GRIEZMAN NA TORRES VS RONALDO NA BENZEMA FAINALI YA UEFA LEO

MATCH PREVIEW: NI GRIEZMAN NA TORRES VS RONALDO NA BENZEMA FAINALI YA UEFA LEO

Picha
Na Mahmoud Rajab Kutoka kuwa local derby mpaka vita kubwa ya makocha wawili, pambano la aina yake lililojaa visasi. Hilo si pambano jingine bali ni la fainali ya Ligi ya Mabingwa kati ya Atletico Madrid dhidi ya Real Madrid litakalopigwa leo kunako dimba la San Siro jijini Milan. Real Madrid wanaingia uwanjani wakiwania taji la 11 wakati Atletico wao wanafanya hivyo kuwania taji lao la kwanza katika historia ya klabu hiyo. Real Madrid wameweka kambani mabao 110 msimu huu na kuruhusu mabao 24 wakati Atletico wameweza kuweka kambani mabao 63 na kuruhusu mabao 18 tu. Unapoziangalia hizi timu mbili basi utagundua Real Madrid ni timu inayoundwa na mastaa walionunuliwa kwa gharama kubwa sana wakati Atletico ni timu inayoundwa na wachezaji wa gharama za kawaida lakini wenye ari kubwa. Vyovyote vile utakavyoungalia mpambano huu, kwanza tambua hili ni pambano linaloashiria kilele cha Champions League, hivyo linabebwa na hisia nzito na linagonga vichwa vya habari vingi duniani. Kwa kuzing...