Lulu Michael Umevuka Mipaka Shika Adabu yako....
KWAKO muigizaji wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, hujambo? Unaendeleaje na shughuli zako za kila siku? Nisalimie mama yako maana naye kitambo kidogo hatujaonana. Ubize huu, we acha tu! Ukitaka kujua afya ya mimi kaka’ko sijambo, namshukuru Mungu. Naendelea kupambana katika eneo langu. Naelimisha, napongeza na hata kukosoa pale ninapoona inafaa. Madhumuni ya barua hii ni kutaka kukuambia ushike adabu kwa watu waliokuzidi umri. Kuna tatizo katika mapitio yako. Kwa umri wako unapaswa kujifunza vitu vingi kutoka kwa wakubwa, hupaswi kupotoka wakati kwanza wewe ni kioo cha jamii. Nilishtushwa sana kusikia umenyanyua kinywa chako na kumjibu vibaya mtu aliyekuzidi umri. Nilijisikia vibaya sana pale mama wa aliyekuwa muigizaji nguli Bongo, Steven Kanumba, Flora Mtegoa alivyokulalamikia kuwa katika majibizano yako na yeye ulikosa staha, ukaweka pembeni aibu, ukafikia hatua ya kumuita kubwa jinga mama huyo. Mama Kanumba yule si kama ma...