Halima Mdee Atupwa Rumande......Mahakama yakana kuzuia uchaguzi wa Meya Dar
Wakati mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee akilala rumande akihusishwa na vurugu zilizotokea Jumapili wakati uchaguzi wa meya wa Jiji la Dar es Salaam ulipokwama, Mahakama ya Kisutu imelikana zuio lililotumika kuzuia shughuli hizo. Uchaguzi huo ulipangwa kufanyika Januari 23, mwaka huu, lakini uliahirishwa ili kuandaa mfumo bora wa upatikanaji wajumbe kutokana na CCM kutaka kuingiza wapigakura nje ya waliotakiwa. Ulikwama tena Februari 8, baada ya Halmashauri ya Jiji la Dar kubaini kasoro ya nyongeza ya majina 14 ya wajumbe kutoka manispaa za Ilala na Kinondoni. Jumapili iliyopita ilikuwa ni mara ya tatu, kukwama tena kutokana na zuio lililosababishwa na kesi iliyofungiliwa na Saad Kimji na Suzan Masawe. Hata hivyo, zuio hilo la muda la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu lililotumika kuahirisha uchaguzi wa meya na naibu meya wa Jiji, uliopaswa kufanyika Februari 27, 2016 limebainika kuwa ni batili. Jana, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Waliarwande Lema alisema Saad K...