WILLIAM MWIJAGE AIWEKA SAWA HISTORIA YA MAREHEMU MOHAMED ALI NA MWALIMU SOMA HAPA LIVE
MWALIMU NYERERE ALIPOMGOMEA MUHAMMAD ALI •Hii ilikuwa ni Jumamosi tarehe 02-Feb-1980 katika uwanja wa ndege wa Dar-es-Salaam (ambao hivi sasa ni Terminal 1) siku bondia Muhammad Ali alipowasili Tanzania. •Katika kilele cha vita baridi (cold war), Muhammad Ali alitumwa na rais wa Marekani Jimmy Carter kuja kuishawishi Tanzania isusie mashindano ya Olympic Games ambayo mwaka huo wa 1980 yalikuwa yanafanyika Urusi (USSR) Moscow kutokana na kitendo cha serikali ya ki-soviet kuivamia kijeshi nchi ya Afghanistan mwaka 1979. •Muhammad Ali, ambaye kabla ya kujiunga na dini ya Black Muslim mwaka 1964 alikuwa anaitwa Cassius Clay, alitumwa kuzishawishi nchi 5 za kiafrika ambazo ni Tanzania, Kenya, Nigeria, Liberia na Senegal. •Utamu wa ziara ya Muhammad Ali uliishia uwanja wa ndege ambapo alipokelewa na watu nyomi wakiongozwa na aliyekuwa waziri wa utamaduni Chediel Mgonja. Labda pia na Kilimanjaro Hotel (hivi sasa Hyatt Regency) alipokaa kwenye ziara hiyo ya siku 3....