Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Siri Kuu Kuhusu Escrow zafichuka

Siri Kuu Kuhusu Escrow zafichuka

Picha
SIRI kuu ya James Rugemalira, kumwaga mabilioni ya shilingi kwa baadhi ya majaji wa mahakama kuu, viongozi waandamizi serikalini na madhehebu ya kidini, wabunge na viogogo wa Ikulu, zimeanza kufumuka.  Nyaraka mikononi mwa gazeti hili zinaonesha zaidi ya asilimia 90 ya wale waliopewa fedha na Rugemalira, ni wale waliomsaidia “kufanikisha ukwapuaji wa zaidi ya Sh. 324 bilioni kutoka Benki Kuu (BoT) na kujinasua katika mikono ya sheria.”  “Rugemalira alishika kila mmoja. Kuanzia Ikulu ya Jakaya Kikwete, TAKUKURU, mahakama, BoT, hazina, ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, viongozi wa madhehebu ya kidini na hata baadhi ya mawaziri wa zamani wenye ushawishi serikalini,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi kutoka Ikulu.  Amesema, “…fedha katika akaunti ya Escrow zilihusisha mtandao mpana ulioratibiwa na Rugemalira na Harbinder Sigh Seth (Singasinga).”  Majaji wa mahakama kuu, Aloycious Mujulizi na Eudeus Ruhangisa, ni miong...