MAUMIVU YA TUMBO
Maumivu ya tumbo ni dalili inayosumbua watu wengi kwa wakati na umri tofauti. Karibu kila mtu katika maisha yake atapata namna fulani ya maumivu ya tumbo. Kuna sababu mbalimbali zinazosababisha maumivu ya tumbo na mara nyingi huwa sio za kutisha, hutubiwa na kupona. Mara chache husababishwa na hali ambazo zinaweza kuhatarisha maisha yako. Maumivu yanaweza kuwa katika sehemu maalum ya tumbo au tumbo zima. Maumivu Ya Tumbo Ni vizuri ukijua aina ya maumivu ya tumbo unayopata pamoja na dalili zinazoambatana nayo. Hii itasaidia kujua sababu ya maumivu na katika matibabu. Maumivu ya tumbo yanaweza kuwa maumivu ya kuchoma, kuungua, kukandamiza, kukata au. Yanaweza kuwa yanakuja na kuacha baada ya muda fulani. Pia yanaweza kuambata na dalili nyingine kama kutapika, kuharisha, kukosa choo, kupata choo chenye damu, tumbo kuvimba na homa. Sababu za Maumivu ya Tumbo Kuna hali nyingi zinazoweza kusababisha maumivu ya tumbo. Chanzo cha maumivu hutegemea na sehemu maumivu yalipo. Maumivu chini ...