Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Ya Nchi

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Ya Nchi , Hamad Yussuf Masauni Alalamikiwa na Wabunge Kwa Kutoa Majibu ya Dharau na Kiburi Kwa Wabunge

Picha
SIKU chache baada ya Rais John Magufuli kutengua uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga kutokana na ulevi, Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Hamad Yussuf Masauni, ameshtakiwa kwa uongozi wa Bunge akidaiwa kutoa majibu ya dharau bungeni. Wakati wizara hiyo bado haijapata Waziri tangu 'kutumbuliwa' kwa Kitwanga Mei 20, mwaka huu, katika Kikao cha 36 cha Mkutano wa Tatu wa Bunge la 11 mjini hapa, jana Mbunge wa Nkasi (CCM), Ally Keissy alisimama na kuomba mwongozo wa Spika akidai Mhandisi Masauni amekuwa akitoa majibu ya dharau kwa wabunge.    Keissy alidai Naibu Waziri huyo amekuwa akitoa majibu ya kejeli na kiburi na kwamba wabunge wengi hawaridhishwi na majibu yake.    "Nasimama kwa Kanuni ya 68(7), naomba mwongozo wako kuhusu majibu ya nyongeza aliyojibu Naibu Waziri, na tangu jana (juzi), amezoea kujibu kwamba wabunge watumie fedha za mfuko wa Jimbo kukarabati majengo ya polisi," Keissy alisema.    "Ndugu Mheshimiwa Naibu Spika...