Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya SAED Kubenea Amkana Paul Makonda Mahakamani....

SAED Kubenea Amkana Paul Makonda Mahakamani....

Picha
SAED Kubenea, Mbunge wa Jimbo la Ubungo pia Mkurugenzi wa Kampuni ya Hali Halisi Publishers amekana kumtusi Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, anaandika Faki Sosi. Kubenea amekana kumtukana Makonda leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Slaam wakati akitoa ushahidi wa kesi inayomkabili kufanya hivyo iliyofunguliwatarehe 15 Desemba mwaka jana. Kwenye kesi hiyo, Kubenea alifungiliwa madai matatu ambayo ni lugha ya matusi, kumwita Makonda mpumbavu, mjinga pamoja na cheo cha kupewa. Katika kesi hiyo iliyopo mbele ya Hakimu Thomas Simba ambayo Kubenea alionekana kuwa na kesi ya kujibu, imeanza kusikilizwa leo baada ya mbunge huyo kuanza kutoa ushahidi wake. Kubenea ndiye shahidi namba moja kwenye kesi hiyo ambapo ameieleza mahakama kwamba, katika vuta nikuvute iliyotokea tarehe 14 Desemba mwaka jana kwenye Kiwanda cha nguo cha TOOKU kilichopo Ubungo, jijini Dar es Salaam hakumtukana Makonda na kwamba, hatua ya kumkatalia kuzungumza na wananchi s...