UDA Yazikwa Rasmi.....Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Yavunja Mkataba
Hatimaye uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, umevunja mkataba wa uwekezaji wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam(UDA) na Kampuni ya Simon Group Limited inayomilikiwa na mfanyabiashara, Robert Kisena. Mkataba huo ambao umekuwa ukipigiwa kelele ndani na nje ya Serikali, umetajwa kutokufuata taratibu za kisheria na kukiuka Sheria ya Manunuzi (PPRA). Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, jana, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita alisema uamuzi huo umefikiwa, baada ya kufanyika kikao halali cha Baraza la Madiwani. Aidha baraza hilo la madiwani pia limeamua kwamba, asilimia 51 ya hisa zilizokuwa zinamilikiwa na kampuni hiyo zirudishwe chini ya uongozi wa jiji hilo. Mwita alisema madiwani walipitia upya mkataba wa uwekezaji kati ya kampuni hiyo na Halmashauri ya Jiji, ambapo walibaini udhaifu katika maeneo mbalimbali wakati wa makabidhiano. Meya huyo anayetokana na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), aliyataja maeneo hayo kuwa ni pa...