Walimu wahofia kudhalilishwa kwenye daladala
Paul Makonda Kwa ufupi 12,562-Idadi ya walimu wa shule za msingi mkoani Dar es Salaa. 4,285-Idadi ya walimu wa shule za sekondari jijini Dar es Salaam Sh270m-Kiasi cha fedha ambacho walimu hawatalipa kwenye daladala iwapo mpango huo utatekelezwa kwa mwezi. Sh800-Wastani wa nauli ya mwalimu mmoja kwa siku kwa kima cha chini Dar es Salaam. Wakati baadhi ya walimu wametoa maoni tofauti kuhusiana na ofa ya kusafiri bure katika mabasi ya daladala jijini Dar es Salaam, imebainika wamiliki wa mabasi, kwa siku watakosa kiasi cha Sh13.4 mpango huo utakapoanza kutekelezwa. Ofa ya usafiri wa bure kwa walimu wa shule za msingi na sekondari zinazomilikiwa na Serikali ilitangazwa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda mbele ya viongozi wa vyama vya usafirishaji abiria na madereva Mkoa wa Dar es Salaam. Katika tangazo lake Makonda alisema kuanzia Machi 7, walimu wa shule za Serikali za msingi na sekondari mkoani Dar es Salaam hawatalipa nauli kwenye daladala wakati wakienda n...