Waziri Mkuu Akutana Na Waziri Wa Biashara Wa Oman
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kuendeleza sekta ya viwanda kama mkakati wa kukuza uchumi ili nchi iweze kutoka kwene umaskini na kufikia uchumi wa kati. Waziri Mkuu amesema hayo leo (Alhamisi, Aprili 14, 2016) alipofanya mazungumzo na Waziri wa Biashara wa Oman, Dk. Ali Masoud Al Sunaidy ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam. Amesema mbali na kuimarishwa kwa sekta ya viwanda, pia Serikali imelenga kuboresha sekta za nishati, uchukuzi na kilimo ambazo zitawezesha Taifa kufikia malengo yake ya kufikia uchumi wa kati. “Sekta ya viwanda ni eneo ambalo tunataka kuliimarisha kwa sababu litatuwezesha kuongeza thamani ya mazao na bidhaa zinazozalishwa nchini jambo ambalo pia litakuza ajira kwa vijana. Hivyo nawakaribisha mje kuwekeza nchini,” amesema. Pia Waziri Mkuu amemuhakikishia kuwa serikali ipo tayari kutoa ushirikiano kwa wawekezaji wa kutoka Oman kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali. Kwa upande wake, Dk. Al Sunaidy amefurah...