MAMBO TISA HUSIYOYAJUA KUHUSU RAISI MKONGWE AFRIKA...ROBERT MUGABE WA ZIMBABWE>
Alizaliwa katika kijiji cha Kutama, kusini-magharibi mwa jiji kuu Harare, alisomeshwa na wayesuti, na baadaye akawa mwalimu kabla kujiingiza katika harakati za kupigania uhuru wa Zimbabwe. Uwanaharakati wake ulimfanya afungwe gerezani kwa miaka 11, na baadaye mwaka 1980 akawa rais wa kwanza wa Zimbabwe. Yafuatayo ni mambo tisa ambayo huenda hukuwa wayajua kumhusu kiongozi huyu-na ambayo huenda yamemuwezesha kuwa rais kwa muda mrefu mno. Mugabe akionekana mwenye furaha mno 1) Zoezi na vyakula vya kienyeji Mugabe anapenda kufanya mazoezi. “Mimi hujihisi mgonjwa wakati sijafanya mazoezi ya viuongo vya mwili,” Bw. Mugabe alisema miaka mitatu iliyopita. Huwa anaamuka kati ya saa kumi na kumi na moja alfajiri, na kutokana na jamaa zake wa karibu, husikiliza BBC idhaa ya dunia. Siri nyingine ya kuishi kwake kwa muda mrefu ni kuwa ywapenda sana-chakula cha kienyeji kinacholiwa sana Zimbabwe. Kisha pia, havuti sigara, ila hunywa pombe kidogo an...