Lema Amwaga Sumu Bungeni Kuhusu Staili ya Utawala wa Rais Magufuli..Adai Taifa Linahitaji Maombi
GODBLESS Lema, Mbunge wa Arusha (Chadema) leo amemwaga sumu bungeni kuhusu staili ya utawala wa Rais John Magufuli, anaandika Faki Sosi. Amesema, kwa namna Rais Magufuli anavyoendesha nchi, taifa linahitaji maombi ya haraka kuhakikisha anarudishwa kwenye mstari wa maadili kwa manufaa ya nchi. Akisoma Makadirio na Mapato katika Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Lema ambaye ni msemaji wa kambi ya upinzani kwenye wizara hiyo amesema, Rais Magufuli ataumiza watu wengi. “Wakati Taifa letu linapita kwenye changamoto nyingi kama vile ukosefu wa sukari, umeme, umasikini, mizigo kupungua bandarini, madini ya Tanzanite kuanguka bei na ubadhirifu uliokithiri katika mfumo wa utawala. Rais mwenyewe ameonekana kufuatilia na kufanyia kazi habari za kwenye mitandao ya kijamii. “Kwa tabia hii ya Rais Magufuli, kama Taifa tunahitaji maombi haraka, kwani Rais ataumiza watu wengi sana kwa kufuatilia maneno ya mit...