Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Dar usiku

Dar usiku, unaweza kudhani ukahaba umehalalishwa

Picha
Kwa hali ilivyo unaweza kusema ukahaba jijini Dar es Salaam umehalalishwa. Hivi sasa wanawake wanaofanya biashara hiyo na wateja wao wamekuwa wakifanya ngono kwa malipo kweupe na katikati ya makazi ya watu bila kificho, huku ikionekana kuwa ni mfupa mgumu kwa Serikali kutokana na sheria kutotambua kama ni halali au la na bali wanaokamatwa hushtakiwa kwa uzururaji. Timu ya waandishi wa gazeti hili, ilitembelea maeneo maarufu kwa biashara hiyo hasa baa na kushuhudia wanawake wanaojiuza na wateja wao wakifanya ngono katika vichochoro vya karibu, katika viti ndani ya baa hizo na kwenye magari. Kadhalika, waandishi walibaini kuwa baadhi ya wanawake wanaojiuza wameolewa waume wao wanajua kuwa wake zao wanajiuza lakini wamewaruhusu ili kutafuta fedha. Hali ilivyo Kinondoni, Temeke, Ilala Katika biashara hiyo, makahaba hao wamebuni mbinu za kuhakikisha hawakosi wanunuzi ikiwamo kuweka mitego katika klabu ambazo hupiga nyimbo za zamani au za ‘watu wazima’ kama ambavyo wenyewe h...