UNDANI WA KIFO CHA KINYAMBE UKO HAPA
Marehemu James Peter Nsemwa ‘Kinyambe’ enzi za uhai wake. WAKATI mwili wa msanii wa vichekesho James Peter Nsemwa maarufu kama Kinyambe ulitarajiwa kuzikwa jana katika Makaburi ya Uyole mkoani Mbeya, gazeti hili limefukunyua na kuupata undani wa kifo chake. Kwa mujibu wa baba wa marehemu, mzee Lugendelo Nsemwa, mwanaye aliyejipatia umaarufu mkubwa kutokana na uwezo wake wa uchekeshaji, alianza kuumwa tangu Juni mwaka jana, ambapo tumbo na miguu ilikuwa ikijaa maji. Alisema tatizo hilo lilisababisha mapafu yake kushindwa kufanya kazi sawasawa. Jeneza lenye mwili wa marehemu Kinyambe. “Kwa kipindi kirefu alikuwa amelazwa katika hospitali binafsi ya Abaja iliyopo Uyole, lakini Mei 9, mwaka huu hali yake ilibadilika, alizidiwa na kupoteza fahamu, kitu kilichotufanya tumkimbize katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya iliyopo maeneo ya Forest ya zamani, ambako alilazwa katika wodi ya ‘private’ chumba cha peke yake na bahati mbaya Jumatano saa 3.5...