TRA WAMTAKA PROFESA TIBAIJUKA KULIPA KIASI CHA SH. MILIONI 500 KUTOKA KATOKA MGAWA WA ESCROW
Hatima ya kesi ya Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka kupinga kuilipa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zaidi ya Sh500 milioni kutoka katika mgawo wa Sh1.62 bilioni zinazohusishwa na fedha zilizochotwa Akaunti ya Tegeta Escrow, itajulikana Machi 29, wakati Bodi ya Rufaa za Kodi (Trab) itakapotoa uamuzi. Tarehe hiyo imepangwa na Makamu Mwenyekiti wa Trab, Hakimu Agusta Mmbando baada ya kukamilika kwa hatua ya usikilizwaji pande zote mbili kwenye kesi hiyo. Profesa Tibaijuka alikata rufaa Trab baada ya TRA kumpelekea madai ya malipo ya kodi ya Sh586 milioni kutokana na mgawo wa Sh1.62 bilioni anazodaiwa kupokea kutokana na fedha zilizochotwa kutoka akaunti hiyo iliyofunguliwa na Shirika la Umeme (Tanesco) na kampuni ya kufua nishati hiyo ya IPTL kwa ajili ya kuhifadhi fedha za malipo ya ununuzi wa umeme wakati mzozo wao ukiwa mahakamani, lakini zikachotwa kwa njia ambayo ilizua shaka. Rufaa hiyo ilisikilizwa na Hakimu Mmbando Februari 17, 19 na 22 wakati Profesa Tibaijuka a...