Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Awaasa Wanafunzi Kuhusu Ajira

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Awaasa Wanafunzi Kuhusu Ajira

Picha
RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, amewasaa wanafunzi kuchagua kozi zitakazowapatia ajira wanapo hitimu masomo yao. Akizungumza katika mahafali ya 10 ya kidato cha sita katika Shule ya Sekondari Baobab, wilayani Bagamoyo, mkoa wa Pwani juzi, Kikwete alisema wimbi kubwa la vijana wasio na ajira limechangiwa na uchaguzi mbaya wa kozi ambazo haziendani na soko la ajira la sasa.    “Nawasaa kuwa makini katika kuchagua kozi zinazoendana na soko la jira ndani na nje ya nchi ili muweze kuajiriwa na kujiajiri pindi mnapohitimu,”  alisema.    Alisema zipo fursa mbalimbali ikiwamo za kibiashara katika soko la Afrika Mashariki, Afrika na Dunia, ambazo kama wahitimu watasoma kozi zinazoendana na fursa zilizopo watajikomboa na changamoto ya ukosefu wa ajira.    “Nimetembea nchi nyingi duniani na kuona fursa mbalimbali, ni vyema basi vijana wakawa wanafanya maamuzi sahihi ili waweze kutumia fursa hizo.”    ...