Binti anayefanya kazi Mochwari atinga Global TV
BINTI mwenye miaka 19, Sabrina Gharib, anayefanya kazi kwa vitendo kimasomo kwenye Mochwari ya Hospitali ya Rufaa ya Tumbi Kibaha mkoani Pwani, amekuwa gumzo kwa watu wanaokwenda kuchukua miili ya wapendwa wao hospitalini hapo, leo ametinga ndani ya mjengo wa Global Publishers na kufanyiwa mahojiano na Global TV Online. Akifanyiwa mahojiano katika kipindi cha Exclusive, Sabrina aliyekuwa ameongozana na mama yake alisema kuwa hajawahi kufundishwa ujasiri na alichokuwa akifanya ni moyo wa kipekee alioumbiwa nao. “Kwa mara ya kwanza nilipoanza kufanya kazi mochwari nilipewa maiti ya bibi, kiukweli nililia sana na sio kwamba nililia kuiona maiti ama kwa uoga bali kwa uzee aliokuwa nao yule bibi, baada ya hapo nikazoea nikawa nahudumia vizuri,’ alisema Sabrina. Mbali na hiyo, Sabrina anayeishi Mlandizi alisema kuwa amekuwa na wakati mgumu kwa kutengwa karibu na marafiki zake wengi kutokana na kazi anayofanya. “Nilikuwa na marafiki wengi lak...