Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Chumba Cha Dereva Tax Chazua Kizaa Zaa Mtaa Wa Mbezi Mtoni Gold Star

Chumba Cha Dereva Tax Chazua Kizaa Zaa Mtaa Wa Mbezi Mtoni Gold Star, Jijini Dar Baada ya Kukutwa Kimejaa Makopo ya MIKOJO na KINYESI

Picha
Na Ripota wa Sufianimafoto ,Dar UKIHADITHIWA na kuonyeshwa chumba cha Dereva Tax anayeonekana kitaani na katika kazi zake akiwa amepiga pamba wala hutaamini masikio yako wala macho yako pindi utakapopata bahati ya kufika na kushuhudia chumba hicho kilichopo maeneo ya Gold Star Mtaa wa Mbezi Mtoni Bondeni jijini Dar es Salaam. Mwandishi wa habari hii alipata fursa ya kufika na kushuhudia yale yaliyokuwa yakisemwa na baadhi ya wakazi wa mtaa huo jana majira ya saa tano usiku baada ya kutokea mtafaruku na sintofahamu katika nyumba hiyo ya Mama Mwakajinga, anayoishi Dereva huyo aliyejulikana kwa jina la Steven al-maarufu kama ‘NYATI’. Akizungumza na mwandishi kuhusu tukio hilo, Mama mwenye nyumba, alisema kuwa siku ya Mei 23, akiwa ameketi uwaji karibu kabisa na Chumba cha Jamaa huyo huku akichambua mboga, alihisi harufu kali na mbaya iliyokuwa ikivuma kutoka chumbani kwa Dereva huyo aliyepanga katika nyumba yake tangu mwaka 2008 na kuona wadudu aina ya funza wakitoka ...