TOO MUCH! NDOA YA OKWI NA SIMBA MPAKA LINI?
Na David Wambura Sasa too much ndiyo unachoweza kusema baada ya duru za kimichezo pamoja na kauli mbalimbali za baadhi ya viongozi wa timu ya Simba SC kuanza kuonesha wako tayari kumrudisha klabuni kwao mshambuliaji wao wa zamani Emmmanuel Okwi, hususan kauli za Mwenyekiti wa kamati ya usajili Simba bwana Hans Poppe hivi karibuni kwenye vyombo vya habari. Hapa naomba nieleweke wazi hakuna asiyejua ubora wa Okwi enzi zake Simba, mimi ni moja ya mashabiki wake wakubwa wa kile amewahi fanya kwenye klabu ya Simba. Ila hofu yangu kwenye harufu ya songombingo hili ni moja tu, nikiiangalia Simba na viongozi wake wa sasa napata picha huenda wameanza kuamini njia pekee ya kutatua changamoto zao ndani ya uwanja ni kurudisha wachezaji wao wa zamani kitu ambacho si mtazamo sahihi kwa maoni yangu na inasikitisha kama kweli huu ndiyo mtazamo kwani walipaswa kujifunza tayari sababu si mara ya kwanza, kwa nyakati tofauti tumewahi kuwasikia kina Kisiga, Owino hivi karibuni Mgosi, Kazimoto. Wacheza...