Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Wadaiwa 16 Waliotorosha Makontena Bandarimni Kuanza Kufilisiwa Leo

Wadaiwa 16 Waliotorosha Makontena Bandarimni Kuanza Kufilisiwa Leo

Picha
Wadaiwa 16 waliokwepa kulipa kodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), baada ya kutorosha kontena za mizigo yao kwenye Bandari Kavu (ICD) ya Azam mwishoni mwa mwaka jana, mali zao zinaanza kukamatwa leo na kufilisiwa. Mkurugenzi wa Mtendaji wa Kampuni ya Udalali ya Yono, iliyopewa kazi ya kufuatilia wadaiwa hao wakiwemo baadhi ambao wamekamilisha malipo, Yono Kevella alisema hayo Dar es Salaam jana. Kevela alisema kuanzia leo wanakaa na vyombo vya dola, kuanza utaratibu wa kukamata na kufilisi mali za wahusika na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria. Kevela alisema hadi sasa hakuna zuio lililotolewa, linazowazuia kutekeleza wajibu wao katika kukusanya madeni hayo. Hata hivyo alisema, wengi wa wadaiwa baada ya kutolewa kwa muda huo wa siku 14, wameonesha moyo wa kulipa. Wadaiwa 16 hawajamaliza madeni Alitaja wadaiwa 16 ambao hawajalipa madeni yao wala kupunguza, ambao watafilisiwa wasipojitokeza kufanya malipo ni Said Ahmed Said Sh 28,249,352.50, Strauss International (45,393,769....