Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya KARIBU XHAKA

KARIBU XHAKA, MGENI MWENYE SODA YAKE.

Picha
Na Richard Leonce Siku moja nilienda kumtembelea rafiki yangu mmoja nyumbani kwake. Nikiwa njiani nikanunua soda ya kopo nikaweka kwenye begi langu, nilipofika kwa rafiki yangu nikakuta ameniwekea soda mezani. Nikacheka sana kisha nikamwambia mimi nina soda yangu. Hiki kisa hakitofautiani sana na usajili wa huyu kijana mwenye umri wa miaka 23 aliyesajiliwa akitokea Borussia Monchengladbach. Umesikia sentensi zake? >>>Mimi ni mchezaji imara, Arsenal imeongeza mtu mwingine anayejua mapambano. Anaongeza kwamba anafurahi kujiunga na ligi ya England kwa sababu kule Ujerumani alikotoka pamoja na kwamba kuna soka la mabavu lakini waamuzi wa kule ni wakali kwa hilo, tofauti na waamuzi wa England ambako ubabe siyo hiyari. Huyu si mwingine, ni Mswiss Granit Xhaka, Mshika bunduki mpya ambaye amegharimu Pounds ambazo hatujawekewa wazi japo ni kuanzia £25M ambazo zinaweza kuongezeka hadi £35M kulingana na kwango na msaada wake kwa timu utakavyokua. Xhaka hatanii anaposema ...