Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Wapinzani Wataka Wabunge wa CCM Wasioongea Bungeni Nao Wanyimwe Posho

Wapinzani Wataka Wabunge wa CCM Wasioongea Bungeni Nao Wanyimwe Posho

Picha
KAMBI Rasmi ya Upinzani Bungeni, imelitaka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwafutia posho wabunge wa CCM  wanaofika kwenye vikao vya Bunge hilo na kukaa kimya bila kuchangia jambo lolote hata kwa maandishi kwa maelezo kuwa hawafanyi kazi. Msemaji Mkuu wa Kambi hiyo, ambaye ni Mbunge wa Momba, David Silinde (Chadema), alitoa pendekezo hilo jana bungeni mjini hapa muda mfupi kabla ya kuwasilisha maoni ya Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni, kuhusu hotuba ya Mapendekezo ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali katika mwaka wa Fedha 2016/17. Hotuba hiyo ya Bajeti iliwasilishwa bungeni Juni 8, mwaka huu na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango. Silinde alisema;  “Kabla ya kutoa maoni ya Kambi ya Upinzani, ninaomba niweke sawa taarifa zinazopotoshwa na kiti cha Naibu Spika kuhusu posho na kueleza kuwa sisi ndio kila wakati tumetaka posho ziondolewe na kupelekwa kwenye shughuli za maendeleo, lakini Serikali imekuwa ikisuasua kutekeleza jambo hil...