Wafanyabiashara ya Sukari Wamchokonoa Rais Magufuli...... Wapandisha Bei Kiholela, Bodi Yakana Upungufu wa Sukari Nchini
SASA ni wazi kwamba wafanyabiashara wa sukari nchini wameamua kuanzisha vita na Rais John Magufuli, kwa kuamua kuficha bidhaa hiyo na hivyo kuadimika katika soko na kupanda bei. Hatua hiyo ya wafanyabiashara imekuja baada ya Rais Magufuli kupiga marufuku uagizwaji holela wa sukari kutoka nje, isipokuwa kwa kibali maalum cha Ikulu Jana Bodi ya Sukari ililazimika kuitisha mkutano na waandishi wa habari na kueleza kile walichokibaini baada ya kuwapo kwa taarifa kuwa bidhaa hiyo imeadimika. Akitoa tamko kwa niaba ya Bodi ya Sukari na wazalishaji bidhaa hiyo, Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero, Ami Mpungwe, alisema tangu Rais Magufuli alipotangaza utaratibu huo wamebaini kuwa baadhi ya wafanyabiashara wameanza kufanya mipango ya kuhujumu taratibu hizo. Alisema wafanyabiashara hao wameamua kuficha bidhaa hiyo ili kuwaaminisha wananchi kwamba sababu kubwa ya kuadimika kwa sukari inachangiwa na uamuzi huo wa rais. Kabla ya uamuzi huo ha...