KUELEKEA UCL FINAL: HIZI NI TOFAUTI ZA REAL MADRID NA ATLETICO MADRID
Na Mahmoud Rajab Kuelekea fainali ya UEFA siku ya May 28 Real Madrid watakuwa wakijaribu kutwaa taji la 11 katika historia ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati, Atletico watakuwa wakijaribu kulitwaa kwa mara ya kwanza mara baada ya kulikosa mara mbili wakifika hatua ya fainali. Mbali ya kuwa katika jiji moja na kupambana kuwania taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid na Atletico Madrid wanatofautiana kwa vitu vingi sana. Real Madrid ni klabu yenye fedha nyingi na yenye nguvu kubwa kiuchumi ambapo pia imejaza mastaa wenye majina makubwa ulimwenguni. Atletico kwa upande wao, ni klabu ambayo inapambana kutokana na nguvu zao wenyewe na kutafuta mafanikio kwa kutumia wachezaji ambao kamwe hawana majina makubwa ulimwenguni, wengi wao wakiwa hawajulikani. Vilabu hivi viwili vinacheza staili mbili tofauti, vile vile wana ‘fan base’ mbili zenye nguvu tofauti. Mtazamo wao tofauti kwenye mchezo wa Jumamosi utakaopigwa jijini Milan kwenye dimba la San Siro, ndiyo utakaoleta ladh...