Magufuli Atahadharishwa kwa Kauli yake ya Bora Kula Mihogo Kuliko Mkate wa Masimango
Baadhi ya wasomi na wanasiasa wamemtahadharisha Rais John Magufuli kuhusu kauli yake ya kupinga misaada yenye mashariti magumu aliyoifananisha na mkate wa masimango. Akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya kwanza ya juu (flyover), inayojengwa katika makutano ya Barabara za Mandela na Nyerere, kwenye eneo la Tazara juzi, Rais Magufuli aliita misaada ya wahisani ‘mkate wa masimango’ na kusema kuliko kula mkate huo ni bora kushindia muhogo. Hiyo ni mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kuzungumzia misaada yenye masharti tangu Shirika la Changamoto ya Milenia (MCC) la Marekani, kusitisha msaada wa Dola za Marekani milioni 472.8 karibu Sh1 trilioni, zilizokuwa zitumike kuongeza kasi ya usambazaji umeme. MCC ilisitisha msaada huo ikilalamikia uchaguzi wa marudio wa Zanzibar uliofanyika Machi 20, ukisusiwa na Chama cha Wananchi (CUF). Akizungumzia kauli hiyo, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa alisema ni jambo jema kwa Watanzania kujiteg...