MTUNGO WA GIGY MONEY WEMA SEPETU HAGUSI
DAR ES SALAAM: Ndani ya muda mfupi wa ustaa wake ambao hauna hata nusu mwaka, muuza nyago (video queen) ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amegeuka habari baada ya kudaiwa kuwa mtungo au msururu wake wa wanaume mastaa, unatishia kuvunja rekodi ya ule wa Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ ambaye kwa sasa anaonekana atakuwa cha mtoto. UMRI MIAKA 19 TU LAKINI… Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya kuaminika kwenye duru za habari za mastaa Bongo, tayari Gigy mwenye umri wa miaka 19, amemuwashia taa Wema (27) ambaye kwa ustaa wake wa miaka kumi tangu alipotwaa Taji la Miss Tanzania 2006/07, anadaiwa ‘kuyeya’ na wanaume zaidi ya kumi hadi sasa. Baadhi ya wanaume waliowahi kuripotiwa kutoka na Wema ni pamoja na wasanii Herry Samir ‘Mr Blue’, Khaleed Mohamed ‘TID’, marehemu Steven Kanumba, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, CK (kigogo),...