Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya TFF Yalaani Kitendo cha Mashabiki wa Simba Kuwarushia Mawe Viongozi na Wachezaji wa Simba Baada Kufungwa na Toto

TFF Yalaani Kitendo cha Mashabiki wa Simba Kuwarushia Mawe Viongozi na Wachezaji wa Simba Baada Kufungwa na Toto

Picha
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limelaani kitendo cha baadhi ya mashabiki wa mpira wa miguu kufanya vurugu mara baada ya mchezo kati ya Simba SC dhidi ya Toto Africans uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.  TFF imesikitishwa na kitendo hicho cha mashabiki wa klabu ya Simba SC, na kusema inalaani kitendo hicho ambacho sio cha kiuana michezo, huku ikiwataka wanachama, washabiki kuheshimu viongozi wa klabu zao waliopo madarakani na kama kuna masuala ya kujadili wakayajadili katika vilabu vyao.  Mashabiki wa klabu ya Simba walifanya vurugu kwa kurusha mawe, wakilenga kuwadhuru viongozi wa klabu hiyo pamoja na wachezaji, magari waliyokuwa nayo baada ya timu yao kupoteza mchezo dhidi ya Toto Africans kwa bao 1- 0.  Jeshi la Polisi baada ya kuwasishi mashabiki kuondoka eneo la uwanja punde tu mchezo ulipomalizika, mashabiki hao walikaidi na kuendelea kurusha mawe hali iliyopelekea jeshi kutumia mabomu ya machozi kuwatanya katika eneo hilo.  Kufutia kiten...