Hizi Ndizo Siri Za Mafanikio Zilizojificha
Ni matumaini yangu unazidi kuelimika kwa namna moja ama nyingine. Katika makala yetu ya leo nitakwenda kueleza kuhusu siri za mafanikio zilizojificha ambazo wengi wetu huenda tukawa tunazijua au tukawa hautuzifahamu pia. Kimisingi siri hizi ndizo zitakazokufanya wewe uweze kutoka hapo ulipo na kuzidi kusonga mbele kwa maana ya kuwa na mafanikio zaidi. Mafanikio ninayaongelea hapa ni yale ya kila sekta aifanyayo mwanadamu. Mafanikio ndio msingi mkubwa kwa kila mwanadamu. Watu wengi huwa tunapata nafasi mbalimbali za kufanya kazi lakini wengi wetu tunashindwa kuzitumia nafasi hizo. Mfano leo hii umepata ajira mahali fulani wengi wetu hufanya kazi ilimradi tu badala ya kuonyesha uzoefu na ubunifu zaidi ulionao. Ngoja nikusimulie kisa kimoja ili utambue siri hizo zilizojificha za kimafanikio; Kuna mwindaji mmoja katika kijiji fulani alikwenda kuwinda wanyama katika msitu ambao upo mbali na makazi yake. Baada ya kuwinda kwa muda mrefu alizunguka sana hu...