Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Watakaolipa mishahara HEWA kuburuzwa Mahakamani

Watakaolipa mishahara HEWA kuburuzwa Mahakamani

Picha
Serikali imesema vigogo wa juu katika utumishi wa umma, watakaobainika kuhusika kwa namna moja au nyingine katika kufanikisha ulipaji wa mishahara hewa, watafunguliwa kesi ya jinai. Aidha, imesema ifikapo Julai mosi, mwaka huu Halmashauri zote nchini ziwe zimefunga na kutumia mifumo ya kielektroniki katika kukusanya mapato yake ya ndani na zimetakiwa kusitisha ukusanyaji kwa njia ya mawakala. Katika hatua nyingine imesema hadi kufikia Machi, 2016, watumishi 90 wamechukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu na wengine kufikishwa mahakamani kwa kukiuka taratibu na sheria za kazi wakiwemo wakurugenzi watendaji (DED) wa halmashauri watano ambao wamevuliwa madaraka. Hayo yalisemwa kwa wakati tofauti na mawaziri wawili katika Ofisi ya Rais, walipowasilisha hotuba za bajeti kwa ofisi zao kwa mwaka ujao wa fedha bungeni mjini Dodoma jana.  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki akiwasilisha hotuba ya ofisi hiyo, alisema kuanzia sasa kiongozi wa serikali ...