Makala asisitiza utafiti zao la kahawa
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makala amewataka wadau wa kahawa kuzingatia utafiti wa zao hiloHai. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makala amewataka wadau wa kahawa kuzingatia utafiti wa zao hilo ili kuongeza uzalishaji na kufufua zao hilo kwa baadhi ya maeneo mkoani hapa.Makala aliyasema hayo jana alipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Zao la Kahawa Tanzania (TaCRI).Alisema maofisa ugani wanapaswa kujifunza namna ya kuimarisha kilimo bora cha kahawa na kutoa elimu hiyo kwa wakulima.Alisema zao hilo limezorota kwa kiwango kikubwa na kusababisha wakulima wengi kuacha kulizalisha. Makala alisema changamoto ya gharama ya pembejeo na utitiri wa kodi, tozo na ushuru, ni jambo la kutazamwa kisera na kufanyiwa uamuzi upya.Mkuu wa programu ya utunzaji bora wa Kahawa, Susan Mbwambo alisema lengo la TaCRI ni kuona wakulima wananufaika na kilimo na kusambaza teknolojia kwa wakati mwafaka kwa wakulima ili kuongeza tija na uzalishaji ubora.