Askari wa UN waanza tena kushirikiana na askari wa Congo
Askari wa kulinda amani na Umoja wa Mataifa wataanza tena kushirikiana na jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika maeneo yenye ghasia na machafuko mashariki mwa nchi hiyo.Afisa wa Umoja wa Mataifa ambaye hakutana jina lake litajwe amesema kuwa, askari wa kikosi cha umoja huo wataanza tena kushirikiana na wenzao wa Congo katika mashambulizi dhidi ya makundi ya waasi huko mashariki wa Congo. Afrisa huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa uamuzi huo umechukuliwa katika mazunguzo ya hivi karibuni ya Katibu Mkuu wa Umoja huo Ban Ki-moon na Rais Joseph Kabila wa Congo.Kipaumbele cha kwanza cha operesheni ya pamoja ya kijeshi dhidi makundi ya waasi ni kushambulia waasi wa Rwanda na wale wanaotoka Uganda walioko katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Ushirikiano na misaada ya kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Congo ulisitishwa Februari mwaka 2015. Maafisa wa Umoja wa Mataifa wanaikosoa serikali ya Kinshasa kwa sababu kwa kuwapa madaraka majenerali wawili wanaotuhumi...