Dk. Shein Apuliza, Auma Wafayakazi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesema dhamira ya Serikali ni kuona watumishi wake wanapata maslahi mazuri zaidi ili kumudu gharama za maisha. Pamoja na dhamira hiyo, hata hivyo, utekelezaji wake utategemea zaidi ukuaji wa uchumi ambao utatoa mapato zaidi kwa ajili ya kugharimia uendeshaji wa shughuli za serikali ikiwemo mishahara, alisema Dk. Shein. Akizungumza na ujumbe wa viongozi wa Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi Zanzibar (ZATUC) ofisini kwake Ikulu jana, Dk. Shein alisema viongozi wa wafanyakazi wanapaswa kuelewa hali halisi ya mapato ya serikali na ugumu unaoambatana na kuongeza maslahi ya watumishi bila kuzingatia mapato halisi ya serikali. “Sisi (serikali) wafanyakazi wametuchagua kuwaongoza na nyinyi (viongozi wa ZATUC) ni hivyo hivyo wamewachagua kuwawakilisha. Kwa hivyo ni viongozi kama sisi; hivyo wajibu wetu ni mmoja tu kuwatumikia wafanyakazi,” Dk. Shein alisema. Rais Shein alitoa wito kw...