Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Rais Magufuli Azungumzia Sakata la Wanafunzi Waliotimuliwa UDOM

Rais Magufuli Azungumzia Sakata la Wanafunzi Waliotimuliwa UDOM, Ashangaa Fedha za Mikopo kupelekwa kwa ‘Vilaza’

Picha
Rais John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli amesema kuwa baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma walioondolewa chuoni hivi karibuni hawakuwa na sifa za kujiunga na masomo chuoni hapo. Akizungumza leo katika uzinduzi wa Maktaba mpya ya Kisasa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Magufuli amewataka watanzania kuweka siasa kando nakuzungumzia masuala ya msingi, huku akiwashangaa wanasiasa waliojitokeza kuwatetea wanafunzi hao. “Nimeshukuru wale vijana wameondoka. Wanasiasa haohao, ‘eti ooh.. hao vijana wamekosa pa kulala.. it’s nonsense’. Taifa letu tuliweke mbele kwanza. Siasa zije nyuma,” alisema. Alisema kuwa baadhi ya wanafunzi ambao walibainika kuwa na elimu ya kidato cha nne waliofeli masomo yao na kuruhusiwa kuendelea na masomo ya elimu ya juu ni watoto wa viongozi. “Ukimchukua mtoto wa form four ukampeleka pale, hata kama atafanikiwa kupata degree… itakuwa ya ajabu. Na baadhi ya watoto...