Mambo Matatu Tuliyojifunza Kutokana na Wimbo wa Snura ‘Chura’ Kufungiwa
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo leo imetangaza kuufungia wimbo wa Snura ‘Chura’ pamoja na video yake. Wimbo huo sasa hautakiwi kuchezwa tena kwenye redio na TV (sina uhakika kama video yake imewahi kuchezwa na TV yoyote). Kwa mujibu wa maelezo kwa vyombo vya habari, Snura ana nafasi ya kuirekebisha video hiyo kitu ambacho nadhani hakiwezekani kwakuwa wimbo nao umepigwa marufuku. Serikali pia imesitisha ‘maonesho ya hadhara’ ya Snura hadi pale atakapojisajili BASATA. “Serikali inawataka wasanii kujiuliza mara mbili kabla ya kubuni kazi zao za sanaa. Wafikirie wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wanazipokeaje? Wavae nafasi ya wale wanaowadhalilisha. Waelewe kwamba sanaa si uwanja wa kudhalilisha watu hata kidogo,” yamesema maelezo ya wizara hiyo. Kwa maelezo hayo inaonesha kuwa Snura ana nafasi ya wazi ya kurekebisha mambo na kuendelea na kazi kama kawaida japo hatoweza tena kuutumbuza wimbo huo uliotrend si tu T...