Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo leo imetangaza kuufungia wimbo wa Snura ‘Chura’ pamoja na video yake.
Wimbo huo sasa hautakiwi kuchezwa tena kwenye redio na TV (sina uhakika kama video yake imewahi kuchezwa na TV yoyote). Kwa mujibu wa maelezo kwa vyombo vya habari, Snura ana nafasi ya kuirekebisha video hiyo kitu ambacho nadhani hakiwezekani kwakuwa wimbo nao umepigwa marufuku.
Serikali pia imesitisha ‘maonesho ya hadhara’ ya Snura hadi pale atakapojisajili BASATA.
“Serikali inawataka wasanii kujiuliza mara mbili kabla ya kubuni kazi zao za sanaa. Wafikirie wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wanazipokeaje? Wavae nafasi ya wale wanaowadhalilisha. Waelewe kwamba sanaa si uwanja wa kudhalilisha watu hata kidogo,” yamesema maelezo ya wizara hiyo.
Kwa maelezo hayo inaonesha kuwa Snura ana nafasi ya wazi ya kurekebisha mambo na kuendelea na kazi kama kawaida japo hatoweza tena kuutumbuza wimbo huo uliotrend si tu Tanzania bali nje ya nchi.
Haya ni mambo ambayo nimejifunza kutokana na uamuzi huu na naamini ni somo kwa wasanii pia.
Youtube si kichaka cha kurundika ‘video chafu’
Snura alijua kuwa Chura ni wimbo wa kuweka mbali na watoto na lazima video yake ingezigusa sharubu za serikali kupitia taasisi zake husika kama vile BASATA, TCRA na zingine. Ndiyo maana alisema video yake ataitoa Youtube peke yake, kama alivyofanya Nay wa Mitego kwenye video yake ya ‘Shika Adabu Yako.’ Ni kwasababu imani ya wasanii wengi ni kuwa mkono wa serikali hauwezi kukufikia iwapo mambo yako utayamalizia mtandaoni tu.
Ni kweli kuwa Chura imtrend sana mtandaoni kutokana na clips za video za wanawake wenye mizigo mikubwa wakiucheza kwa madaha. Hakuna anayeweza kubisha kuwa clips hizo pamoja na video yake rasmi imekaa kushoto kimaadili hivyo si jambo la kushangaza serikali kucharuka – ni kitu tulichokitarajia.
Lakini cha muhimu ambacho wasanii wanatakiwa kujifunza ni kuwa si salama tena kufanya kitu controversial ukitegemea kuwa utakiweka Youtube na hakuna atakayejali. Tupo katika nyakati za hatari zaidi sasa hasa kutokana na kupitishwa kwa sheria ya makosa ya mtandaoni ambayo pornography ni kitu chenye adhabu kali huko.
“Serikali inawakumbusha wananchi wote kutojiingiza katika makosa ya sheria ya mtandao kwa kusambaza wimbo huu kwa njia yoyote ile ya kimtandao,” imeonya taarifa ya wizara hiyo. Japo sheria hii haijawa kali sana kwa sasa, bado wasanii wanaweza kupoteza mengi kama wakiamua kufanya vitu vinavyokiuka maadili kwa matarajio kuwa Youtube, Instagram au WhatsApp ni kimbilio na hakuna anayejali.
BASATA haina meno tena?
Awali tulikuwa tumezoea uamuzi wowote wa kufungiwa wimbo au msanii unafanywa na baraza la sanaa la taifa, BASATA au TCRA kwenye matukio machache. Lakini sasa uamuzi huo umechukuliwa na wizara yenyewe, kitu ambacho kimesababisha maswali mengi kuwa iweje uamuzi wa kuufungia wimbo wa Snura umechukuliwa na mamlaka ya juu zaidi! Pengine kuna mabadiliko ambayo sasa yanaifanya wizara kuingia front yenyewe! Hata hivyo kwenye mkutano na maofisa wa BASATA walikuwepo kama watu walioitwa kusikiliza tu.
Video chafu zinaharibu brand
Well, wanasema sex sells, hilo haliwezi kupingwa na ndio maana video nyingi za muziki zenye wasichana warembo wenye vichupi zina views nyingi Youtube. Lakini mara nyingi msanii anapojikuta kwenye mikasa ya kufungiwa kazi zake kwa kigezo cha ‘maadili’ hasa kwa kazi zinazofanana na Chura ya Snura humharibia sifa msanii na brand yake. Matokeo yake katika jamii msanii huyo huanza kuchukuliwa kama ‘aliyeshindikana’ au ‘mhuni’ na kama ikitokea mara nyingi, kibiashara hasa zile kubwa na zinazohusisha makampuni humwathi
Chanzo:Bongo5