Unataka kuacha sigara ?..... fuata njia zifuatazo!
Je, unataka kuacha kuvuta sigara? Sawa, nakubaliana na wewe lakini unajua kwa nini unataka kuacha tabia hiyo ambayo umeizoea kwa muda mrefu?. Kwa sababu haitoshi tu utake kuacha kuvuta sigara bila kuwa na sababu muhimu inayokusukuma uache suala hilo. Kwa hivyo kwanza anza kujiuliza kwa nini unataka kuacha sigara. Kujua sababu kutakusaidia katika kutekeleza lengo lako vyema. Je, unaacha sigara kwa kuwa unataka kuilinda familia yako isipate madhara ya sigara unazovuta? Je, unataka kuacha sigara kwa kuwa umeogopa kupata kensa ya kifua? Au je, ungependa kuonekana kijana zaidi? Tafuta sababu muhimu ambayo itaizidi hamu yako ya kuvuta sigara. Jua kuwa ni jambo gumu kuacha tabia uliyoizoea kwa muda mrefu mara moja. Haitowezekana utupe kipande chako cha sigara yako mara moja na kutangaza kuwa umeacha kuvuta. Suala hilo ni gumu kwani asilimia 95 ya watu wanaojaribu kuacha sigara kwa mtindo huo hushindwa, inabidi upate ushauri na tiba mbadala ili kukusaidia kuacha kuvuta sig...