Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Mkuu Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Afungwa Mwaka Mmoja kwa Kosa la Kuajiri Watumishi Wenye Elimu ya Darasa 7

Mkuu Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Afungwa Mwaka Mmoja kwa Kosa la Kuajiri Watumishi Wenye Elimu ya Darasa 7

Picha
MKUU wa Chuo cha Uhasibu (IAA) Njiro mkoani Arusha, Profesa Johannes Monyo amehukumiwa kifungo cha nje kwa sharti la kutofanya kosa lolote ndani ya mwaka mmoja. Hukumu hiyo ilitolewa Ijumaa iliyopita na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha, Devotha Msofe baada ya kujiridhisha kuwa Profesa Monyo alifanya makosa ya kuajiri watumishi wanane wenye elimu ya darasa la saba bila kufuata misingi na kanuni za utumishi wa umma. Hakimu Msofe alisema Profesa Monyo akiwa Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Njiro, aliwaingiza watumishi wanane kwenye ajira ya kudumu bila ya kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi au Katibu Mkuu Utumishi. Alisema kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani kwa mashahidi 10 pamoja na vielelezo vinane vilivyotolewa mahakamani hapo na upande wa mshtakiwa kuwa na mashahidi wawili, mahakama hiyo imejiridhisha pasipo shaka kuwa Profesa Monyo alifanya kosa hilo la kuajiri wafanyakazi hao wanane bila kufuata taratibu za kisheria. “Mahakama imejiridhisha pasipo shaka kuwa ulif...