Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Mtu 1 ameuawa kwa risasi na kusababisha vurugu kati ya polisi na wananchi mkoani Mara.

Mtu 1 ameuawa kwa risasi na kusababisha vurugu kati ya polisi na wananchi mkoani Mara.

Picha
Watu kadhaa wakiwemo wagonjwa waliokuwa wamelazwa katika kituo cha afya cha Nyamongo wilayani Tarime mkoani Mara    wamejeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi za moto wakati askari wa jeshi la polisi wakipambana na baadhi ya wakazi wa mji huo walikuwa wakiwazuia polisi kuchukua mwili wa kijana mmoja anadaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na askari wa jeshi la polisi. Tukio hilo ambalo limesababisha wagonjwa watatu ambao wamelazwa katika kituo hicho cha afya maarufu kama hospitali ya Sungusungu kujeruhiwa vibaya kwa kipigwa risasi, imeelezwa na baadhi ya viongozi wa vijiji katika eneo hilo kuwa askari polisi walianza kurusha risasi baada ya kutofautiana na familia katika kuchukua mwili wa kijana huyo Jackison Mwita. Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Tarime vijijini Mh John Heche ambaye ametembelea mji wa Nyamongo kufuatia tukio hilo, ameonesha kusikitishwa kwa askari polisi hao kuua wananchi kwa risasi kisha   kusababisha vurugu hizo ambazo pia zimesababisha uharibifu mkubwa ...