Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya DARAJA la Kigamboni Laanza Kutumika Kwa Mbwembwe...Wengine Wafanya Kama Sehemu ya Kivutio

DARAJA la Kigamboni Laanza Kutumika Kwa Mbwembwe...Wengine Wafanya Kama Sehemu ya Kivutio

Picha
Baada ya Serikali kuruhusu matumizi ya daraja jipya la Kigamboni kwa watembea kwa miguu na magari kwa majaribio, hatua hiyo imepeleka neema kwa wakazi wa mji huo, huku ikipunguza idadi ya vyombo vya moto katika vivuko.  Jana asubuhi, mwandishi wetu alishuhudia magari yakipita katika daraja hilo, kama ilivyo katika barabara zilizozoeleka za Mandela na Morogoro, huku baadhi ya madereva wakiendesha na kujipiga picha kwa simu za mkononi.  Watembea kwa miguu nao hawakuwa nyuma na idadi yao ilizidi kuongezeka mchana baada ya mvua zilizokuwa zikinyesha kuisha na sehemu kubwa walionekana kama watalii waliokuwa wakipiga picha na kuzunguzunguka katika eneo hilo.  “Sasa hivi mtu anakuwa na chaguo apite wapi anapoona atafanikisha safari yake kulingana na mahitaji,” alisema mmoja wa madereva waliotumia daraja hilo, Emmanuel Nzera.  Alisema kufunguliwa kwa daraja hilo ni neema kwa kuwa litaondoa usumbufu wa foleni katika vivuko upande wa Kigamboni na Feri na kwam...